- KATIKA maisha mawazo ni kitu cha kawaida kwa mwanadamu,
lakini hata hivyo matumizi ya akili lazima yawekewe mipaka na isiwe ni
kitu cha kawaida ubongo kuruhusiwa kwenda mwendo mkali kulingana na
uwezo wake.
-
- Waundaji wa mashine kwa mfano, wakati wanatengeneza injini waliweka
mwendokasi wa kiwango cha juu, hata hivyo wanaonya siyo kila wakati
mwendesha chombo ana ruhusa ya kutumia spidi yote iliyomo ndani ya
mashine yake.
-
- Hali hiyo ndiyo inayojitokeza katika uwezo wa ubongo kufikiri na
kupata majibu ya kina ya nini kilichopo na kitakachotokea. Ni ukweli
ulio wazi kwamba ubongo ni mashine kubwa yenye uwezo wa ajabu
usioelezeka.
-
- Watu wengi waliofanikiwa na wanaotaka kufanikiwa ni wale ambao
wanajua namna ya kuutumia ubongo katika kupanga maisha yao. Kila
unachokiona ni zao la ubongo kwani mawazo ndiyo mwanzo wa kila kitu
kilichopo duniani. Binafsi naamini hata Mungu aliwaza kabla ya kuumba
ulimwengu.
-
- Lakini pamoja na umuhimu wa mwanadamu kutumia akili yake kupata
majibu ya hisia, maono, mazingira na vitu anavyokutananavyo maishani,
kuna wakati umuhimu huo unakosa maana na maonyo ya kuwa na udhibiti kasi
ya fikra yanachukua nafasi. Haijalishi mhusika ana uwezo wa kiasi gani
ndani ya akili yake! Kumbuka pia onyo la dereva kutumia mwendokasi kila
anapowasha gari lake, halafu linganisha na akili yako au ya mwanadamu
unayemtazama utagundua kuwa kidhibiti mwendo kinahitajika hata katika
mawazo. Hebu chukua jukumu la kuutazama ulimwengu huu tulio nao na
uangalie uozo wa wanadamu katika kujiheshimu, kisha ujiulize hivi kuna
mwanaume au mwanamke anayeishi bila kumsaliti mpenzi wake?
-
- Baada ya swali hilo wachukue rafiki zako unaokunywa nao pombe na
kufanya nao kazi uone kama hamjawahi kuoneshana nyumba ndogo, baadaye
fumba macho uiulize akili yako kuna asiyesalitiwa? Bila shaka kwa
mchakato huo mfupi tu majibu ya haraka yatakayokuja ni hakuna mwenye
imani ya asilimia mia moja ya kusalitiwa isipokuwa kuna kuuficha ukweli.
Sasa kwa majibu hayo ya akili, mkeo unampenda nini wakati unahisi
anatoa penzi kwa wanaume wengine kama wewe?
-
- Thamani ya ndoa na umuhimu wako unatoka wapi? Tuseme hupati uchungu
pale unapohisi unaibiwa mumeo? Kama unapata inakuwaje pale akili
inapokupa majibu kuwa mkeo si mwaminifu? Hapa ndipo penye kiini cha somo
letu kwamba, kuna wakati tunaruhusu mawazo yetu yakimbie mwendokasi
kwenye njia yenye mabonde na kona na wengi wetu tumeharibu ndoa zetu na
wengine tumeachana na wapenzi wetu kwa ujinga wa kutozuia kasi ya akili
zetu.
-
- Inashangaza kusikia na kuona kuna baadhi ya wanandoa wanaishi kwa
kupelelezana kila siku kama askari wakaguzi wa dawa za kulevya. Mke
akichelewa kurudi lazima akaguliwe kwanza kama hakutoka kupasha mwili
nje, kadhalika mwanaume apimwe kwa kunuswa kama hakuchepukia nyumba
ndogo.
-
- Hivi tulishawahi kujiuliza kuwa tunautumia ubongo wetu vibaya
kutafuta ufumbuzi wa mambo ya kipuuzi? Tunawafuatilia wake zetu
maofisini mwao ili iweje? Hatuaminiani kwa nini wakati tumeoana? Je
mapenzi yana faida gani ndani ya usaliti na kujua kuwa siyo wewe peke
yako unayefaidi tunda la mkeo au mumeo?
-
- Wakati nikitafakari kuhusu mada hii kaka mmoja aliniambia kuwa
amempata mchumba ambaye ni mzuri sana, anampenda na kumheshimu, lakini
alitaka kujua atawezaje kumwamini kuwa hatamsaliti? Kabla sijamjibu
akajaza hoja nyingine kwamba kuna watu kibao wanamsumbua mchumba wake
kwa maana hiyo ana shaka kuna siku atalegeza msimamo na kumsaliti!
Binafsi sikufikiria sana kumjibu swali lake, bali nilimwambia kuwa jibu
la swali lako ni kujimilikisha ujinga.
-
- Nikiwa na maana ileile ya kudhibiti mwendo wa akili yake kwa kuacha
kuwaza mambo yanayoashiria kutumia mwendo kasi wa akili kwenye njia
mbaya. Siku zote kushinda maisha kunahitaji uwezo wa mwanadamu wa kujua
ni wapi awaze sana na kupata ufumbuzi, wapi awaze kidogo au asiwaze.
-
- Maana haiwezi kuwa busara kwa mtu aliyemfuma mkewe na mwanaume
mwingine atumie akili kujua ilikuwaje wakati mpaka kukawepo makubaliano
au msukumo upi ulimvuta mkewe kujifunua kwa mwingine? Inapofikia hatua
hiyo umuhimu wa kulegeza mwendo wa akili kwa kusema sijui na sina haja
ya kujua ilikuwaje, hata kama akili bado inao uwezo wa kujua mengine
zaidi sema sitawaza juu ya jambo hili la kipuuzi!
-
- Ukifanya hivyo utakuwa sawa na dereva anayeendesha gari lenye injini
yenye kasi kubwa lakini ameamua kwa makusudi tu kupunguza mwendo kwa
usalama wa maisha yake.
-
Hii ndiyo siri ya usalama wa ndoa na uhusiano wa mapenzi ndani ya
hofu ya usaliti. Ukiona mawazo yanakuja kutaka kutoa jibu la kuchelewa
kwa mumeo kurudi huku dondoo za kuwepo kwa msichana mwingine kazini
kwake zikichipuka, yatupilie mbali mawazo hayo
source.. https://globalpublishers.co.tz/
Comments
Post a Comment