Skip to main content
Diamond Afunguka haya kuhusu wimbo wake...soma zaidi..by nasanyo fortnine
Diamond afafanua sababu za kuachia wimbo ‘Acha Nikae Kimya’ uliogusia suala la Roma
- Diamond
Platnumz ameachia wimbo wake mpya kwa kushtukiza uitwao ‘Acha Nikae
Kimya.’ Wimbo unazungumzia masuala mengi yanayotokea sasa ikiwemo hofu
iliyotanda baada ya Roma na wenzie kutekwa. Wimbo huo hata hivyo
umepokelewa kwa hisia tofauti.
- Ili nchi ipate maendeleo inahitaji
Upendo na Ushirikiano wa Wananchi na Serikali..Na Nikiwa kama Msanii,
jukumu langu ni kuhakikisha natumia Hekma na busara kukemea jambo
nilionalo haliko sawa ili lirekebishwe, lakini pia panapokuwa hakuna
maelewano jukumu langu pia ni kupatanisha ili kwa pamoja tujenge nchi
yetu kusudi wazazi wetu, watoto pamoja na familia zetu waishi kwa Upendo
Amani na kufurahia nchi yetu…Na ndiomaana kwenye nyimbo nakwambia “MI
NA WEWE WA TAIFA MOJA…KAMBARAGE BABA MMOJA….SASA TOFAUTI ZA NINI
TUSHIKAMANE TUKAIJENGE TANZANIA”… Unatakiwa utambue kuwa kila kiongozi
ni Binadamu na kama wote tujuavyo, Binadamu hatujakamilika… hivyo katika
nchi yoyote lazma wakati mwingine kuna jambo linaweza likawa haliko
sawa, ila sisi kama wananchi tunatakiwa tutumie Hekima na Busara kwenye
kufikisha ujumbe ama hoja zetu ili viongozi walieke sawa…Busara na
Hekima itafanya viongozi watuelewe kirahisi na pengine mengi tuyatakayo
tutimiziwe kirahisi… mfano mzuri, juzijuzi kupitia kipindi cha Clouds360
cha clouds Tv nlipopata bahati ya kuongea na Mh Raisi nilimuomba
atufungulie Mabanda ya Chipsi na Bodaboda ziruhusiwe kufanyakazi hadi
asubuhi maana zilikuwa nwisho saa 4 ama 5 usiku…kwakuwa nilitumia Hekima
na busara kwenye Kufikisha hoja ama Ombi langu..alikubali na tukapewa
ruksa na sasa hivi maeneo mengi ya Chipsi na Bodaboda yanafanya kazi
hadi usiku mnene… hivyo tusikubali tu kulishwa Sumu za kuleta ugomvi
kati yetu wenyewe kwa wenyewe eti Mara Tutukane mara sijui fanyeni hiki,
wakati hata baadhi ya wanaochochea mambo hayo hawaishi Tanzania
wanaishi Ulaya / Marekani / kifupi nje ya nchi…ikija kutokea bahati
mbaya kimenuka wao watakuwa wanakula kuku kwa mrija huko walipo…halafu
sisi na familia zetu ndio tutateseka na kuhaha kunusuru roho zetu usiku
kucha.. Hatutaki makelele ya uchonganishi mitandaoni.
-
- cc #africaswahilitv
Comments
Post a Comment