ALICHOSEMA IDRISS SULTAN KUHUSU ROMA NA WENZAKE SOMA ZAIDI

HAYA NDIYO ALIYO YAANDIKA IDRISS SULTAN KATIKA UKURASA WAKE WA INSTAGRAM
  • idrissultanHawa ni wasanii na ni maarufu, sitamani kujua ni wangapi tusiowajua waliopotea katika mfumo kama huu. Nina hofu sio kwa maisha yangu na uhuru wangu ila kwa kaka, dada, watoto, baba, mama na ndugu , wake, waume, na wapenzi wa watanzania wenzangu wasio na sauti niliyo nayo mimi. Mwenyezi Mungu hakunipa nilichonacho ili niishie kupimisha misuli na wenzangu nani zaidi, watu kama mimi ndio wa kwenda motoni haraka zaidi tukishaulizwa ulifanyia nini ulichopewa. Raisi Magufuli, waziri Mwakyembe, waziri Mwigulu na Mkuu wa mkoa Makonda nina imani hili lipo mezani kwenu naombeni mlitolee tamko zaidi ya "Uchunguzi unafanyika" na pia mlivalie njuga kuwapata ndugu zetu ili kutuliza amani ya hii nchi iliyopiganiwa iliyokuzwa kwa upendo na amani ya juu kabisa. We can't call it the land of peace wakati ukilala hujui kama utaaamka sehemu unayoijua na ukiwa hata na hali yako ya kiafya ile ile. Leo ni Roma na Moni, kesho ni nani ? Kamanda Sirro sijasahau kabisa usalama wa huu mji upo mikononi mwako. Wake za hawa wawili wanaongea na watoto wao wanawaambia baba yupo ila amesafiri anarudi kesho. Kesho isipofika basi inshaallah tutajua Tanzania yetu ni nchi ya aina gani. Hata Mungu simuachii hili hatujalishindwa bado #FreeRoma #FreeMoni



Comments