Skip to main content
WENYE MASHINE ZA KUBETI KUKAMATWA SOMA ZAIDI HAPA
-
-
- MKUU wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ali Hapi ameiagiza
Ofisi ya Biashara ya Manispaa hiyo kushirikiana na Polisi kufanya
operesheni katika vibanda vya michezo ya kubashiri “betting” na
kuwakamata wanaowaruhusu watoto kushiriki michezo hiyo.
-
- Mbali na kuwakamata wamiliki hao, pia amemuagiza Ofisa Biashara wa
Manispaa hiyo, Mohamed Basama kuwasiliana na watoa leseni za mchezo huo
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kuhakikisha wanafuta leseni za wote
watakaobainika kuwaruhusu watoto kucheza mchezo huo.
-
- Agizo hilo limekuja baada ya mkuu huyo wa wilaya kupokea malalamiko
kutoka kwa wananchi kuwa watoto wao wamekuwa wakishindwa kusoma na
wengine kujihusisha na wizi ili wapate fedha za kubeti.
-
- Alisema baadhi ya watoto wamekuwa wakishinda katika vibanda vya
kubeti kuanzia asubuhi hadi usiku, hivyo kusababisha washindwe
kuzingatia masomo yao shuleni.
-
- "Fanyeni operesheni mkikuta watoto katika hayo mabanda ya kubeti,
wakamateni wamiliki wa hayo mabanda mmuwasiliane na idara inayohusika
kutoa leseni, mfute leseni zao na hiyo ndiyo dawa," alisema Hapi.
-
- Aidha, alisema wapo watoto wengine wamekuwa wakishinda kwenye sehemu
zinazoendesha michezo ya kamari kinyume na sheria, ambapo aliagiza pia
watu hao wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
-
- Hapi alionya kama wazazi wasipokuwa makini kutoa taarifa juu ya
vibanda ambavyo watoto wanaingia kushiriki mchezo huo, watatengeneza
kizazi cha wajinga, kitu ambacho hawatakiwi kuruhusu kitokee.
-
- “Unakuta watoto wanaingia darasani lakini vichwani mwao inapita
mashine za kubeti tu, hata ukimuuliza saba mara mbili ngapi hajui. Tena
wengine wana madude feki, mkiyakuta ng'oeni na muwapeleke nayo
mahakamani hivyo ndio vidhibiti," alisema.
-
- Awali akijibu malalamiko hayo, Basama alisema wamekuwa na changamoto
kutokana na kwamba wao hawahusiki na utoaji wa leseni za biashara hizo
na kuahidi watafanyia kazi maagizo ya mkuu huyo wa wilaya.
-
- Akitoa malalamiko katika mkutano huo uliofanyika Kata ya Kinondoni,
mkazi wa mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina la Sophia alisema, watoto
wao wamekuwa hawafiki shule na badala yake kuishia katika maeneo hayo.
-
- “Yaani hata hela zetu ndani hazikai, ukiweka hela kidogo tu unakuta
haipo ameshachukua anaenda kubeti, mheshimiwa tunaomba utoe maagizo
kuhusu hii michezo ya kubeti ni hasara kwa watoto wetui," alisema mkazi
huyo.
Comments
Post a Comment