Skip to main content
POLISI AKAMATWA KISA soma hapa by nasanyo fortnine
- Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon
Sirro, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo ambaye
alimtaja kama Elius Msigwa aliyekuwa akiwababaisha wananchi wa maeneo ya
Kivule anakoishi, alifukuzwa kazi tangu Disemba mwaka jana.
-
- Alisema wakati mtuhumiwa huyo anafukuzwa ndani ya jeshi hilo, alikuwa
na cheo cha Koplo, lakini alipokamatwa alikuwa amevaa cheo cha Sajenti
na alikiri kuwa alifanya hivyo kutokana na kukosa nauli ya daladala.
-
- Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwa nia ya kuomba radhi,
kijana huyo ambaye alikuwa akifanya kazi katika gereza la Keko, alisema
“Bahati mbaya siku ya juzi sikuwa na nauli ya kwenda mjini ndio nikavaa
hizi ‘uniform’ (sare). Nilikuwa nawaomba vijana wenzangu hata kama
umeacha kazi, umefukuzwa au chochote, msivae ‘uniform’ na baada ya
kutoka hapa nazirudisha hizi uniform katika kituo changu kilichokuwa cha
kazi,” alisema Msingwa.
-
- Kamishina Sirro pia alisema jeshi hilo lilikamata watu watatu
wanaodaiwa kuwa ni majambazi katika maeneo ya Kivule, Ukonga
wakijihusisha na wizi wa kutumia silaha aina ya mapanga, kuvuta bangi na
kunywa gongo.
Comments
Post a Comment