Mwanajeshi wa
zamani aliyekuwa amependekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa
mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa amekataa kazi hiyo.
- Robert Harward alitarajiwa na wengi kuchukua wadhifa huo ulioachwa na Michael Flynn aliyefutwa kazi na Bw Trump Jumatatu.
Bw Flynn alimpotosha makamu wa rais Mike Pence kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi nchini Marekani ambayo aliyafanya kabla yake kuteuliwa rasmi kuwa mashauri.
- Pigo hilo kwa Bw Trump, la kukataliwa kwa uteuzi wake na Harward, lilitokea saa chache baada ya Bw Trump kupuuzilia mbali ripoti kwamba utawala wake umekumbwa na mtafaruku mkubwa.
Comments
Post a Comment