Skip to main content
KUFANYA NGONO KWA MDOMO NI HATARI KUBWA SOMA HII
- Utafiti unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia
mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili, pombe kali, vitu
vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi. Utafiti unaonyesha
watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
-
- Katika utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake
wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku
wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270
kutokana na ugonjwa huo. Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya
vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya
kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi
wao katika kushiriki ngono.
-
- Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na
ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui
athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo
kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya
hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na
kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
-
- Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya koo ni ya pili katika
mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume nchini, ikiongozwa na ile ya
ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna
saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
-
- Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani
ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na umri mkubwa
ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama
ile ya ngono ya mgomo.
-
- “Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na
ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo
zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze kumvutia mwanamke
anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo
kabisa,” anasema Dk Kahesa na kuongeza.
-
- “Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua
madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na
mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo
wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama
wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
-
- Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo,
vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kuangalia video za ngono na
staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi
ya ngono ya mdomo.
-
- Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa saratani nchini
wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo kuna kila sababu kwa vijana
kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu wazungu ambayo
mara nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
-
- Anasema katika mtiririko wa saratani zinazoongoza nchini saratani ya
koo inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi wanaopatwa na ugonjwa huo ni
watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na kuendelea hiyo inaonyesha kuwa
wengi wao walianza ngono ya mdomo muda mrefu wakati wakiwa bado wadogo.
-
- “Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini,
inawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na
wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado
wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,” anasema Dk Kahesa.
-
- Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya koo; aina ya kwanza ni
“Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma, zote hutofautiana
wakati zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu yake yanafanana. Aina
hizo ndizo zilizopo nchini na huanza mapema kuharibu seli ambazo zipo
katika utandu uliopo katika ukuta wa koo kabla ya kuenea katika maeneo
mengine ya koo.
-
- Visababishi vya kansa ya koo:
Moja kati ya vitu vinavyosababisha kansa ya koo ni mwenendo wa maisha
yetu kwa kula vyakula vyenye asidi, vyakula vichachu, vyakula vyenye
pilipili, pombe kali na vyakula vigumu ambavyo hukwaruza koo na hivyo
kusababisha saratani.
-
- Anasema asilimia 90 ya wagonjwa wanaopokelewa katika Taasisi ya
Saratani ya Ocean road wanakuwa na historia ya kutumia vikali kama
pombe kali, kuvuta sigara kwa kupindukia, kula pilipili kwa wingi na
kutumia vitu vyenye uchachu.
-
- Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za mgonjwa wa saratani ni chakula kukwama kwenye
koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu
kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate.
-
- Ugonjwa huo unachukua muda mrefu kugundua na kuona viashiria kwani
mwanzo mgonjwa huanza kupata shida kumeza chakula na kwamba wagonjwa
wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya Saratani wanakuwa tayari
wamechelewa kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.
-
- “Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri siku zinavyokwenda ndiyo
kunakuwa na dalili zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu anakuwa na
maumivu wakati wa kumeza chakula, maumivu katika kifua na mgongo na hata
kupungua uzito pamoja na kikohozi kikavu kinachoweza kudumu mwezi
mmoja,” anasema.
-
- Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuhawi hospitali ili aanze
matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa anayewahi kupata
matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye amechelewa
kugundulika na kuanza matibabu.
-
- Kama saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo vyote vilivyopo jirani
na koo na hadi kufika katika tezi au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa
anaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa
maalumu ambacho ni kemikali.
-
- Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya tafiti zinazohusiana na ugonjwa huo
na kusema kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992 kulikuwa na kati ya watu 546
waliopimwa, wanaume 430 na wanawake 116 waligundulika kuwa na ugonjwa
huo.
-
- Utafiti huo ulishirikisha watu wenye umri wa miaka 21 hadi 90,
ulibaini kuwa wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa miaka 50-59 tofauti
na hali iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo unawaathiri vijana wenye
umri wa miaka 40.
-
- Dk Kahesa anasema katika kipindi cha miaka saba iliyopita takwimu za
taasisi yake imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167 hadi kufikia wagojwa
277. Hali inaonekana huenda ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi
wa watu wanaonekana kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za kutumia
midomo.
-
- Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye ananyonya au
kulambana sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa gonoreha, ambapo ugonjwa
huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au
maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea katika
viungo vya uzazi. Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao huambukizwa
kirahisi zaidi kupitia mdomo na hasa pale inapotekoa mdomo unapokutana
na kiungo chenye athari hizo.
-
- Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja wapo kati ya magonjwa ya zinaa
ambao huambukizwa kwa bakteria na kwamba ugonjwa huu pia huambukizwa
kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna
dalili kwa muda mrefu.
-
- Hepatitis A: Hiki ni ni kirusi kinachopatikana katika kinyesi cha
binadamu, kirusi hiki huwaingia wale wanaopenda kunyonya na kulambana
sehemu za haja kubwa. Ni kwamba kwa ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika
macho hadi kupofuka.
-
- Hepatitis B: Ugonjwa huu huambukizwa kama virusi vya Ukimwi kwa
sababu virusi vyake hukaa katika majimaji yanayotoka katika sehemu za
siri na damu. Mtu akiwa na ugonjwa huu, mwili wake unakuwa na vipele
vingi na hata majipu ambayo huwa magumu kupona na wapo wanaokufa.
Vile vile ugonjwa wa Hepatitis C: ni ugonjwa ambao hupatikana pindi damu
inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu. Ugonjwa huu
humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
-
- Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana raha kwa kunyonyana sehemu za
siri, kuna uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi vya Ukimwi kwa
uchache lakini kwa nchi zilizoendelea wamebuni aina ya kondom ambazo
huvaliwa katika mdomo wa binadamu na hivyo kupunguza hatari ya kupata
madhara hayo.
-
- JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema hakuna utafiti wa moja kwa moja unao onyesha kuwa
baadhi ya wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na
upungufu wa nguvu za kiume.
-
- “Utafiti wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha kuwa baadhi ya wanaume
wanafanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na ukosefu wa nguvu za kiume,
hivyo kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili kubaini kama tatizo
hilo lipo licha ya kuwepo kwa kesi nyingi zinazodaiwa kuwa baadhi ya
wanaume hawana nguvu za kiume na wapenzi wao huwafichia siri kwa kufanya
nao mapenzi kwa njia yam domo”anasema.
-
- NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na saikolojia wanasema kuna njia nyingi za
kuandaana wakati wa tendo la ndoa tofauti na kunyonyanyana sehemu za
siri.
-
- Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke kunyonyana
sehemu za ndoa mwenzake na kwamba staili hizo ni staili za wanzetu wa
nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili hiyo ya
kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni
kutokana na kasi ya utandawazi.
-
- Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu huiga staili hizo
kutoka katika mitandao bila kujali kuwa kuna zina madhara makubwa, hivyo
ni jukumu la kila mtu kulinda afya yake na ya mwenza wake. Sio kila
kitu kinachowekwa katika mitandao ya kijamii kina manufaa la hashaa!
vitu vingine vinachangia kuhatarisha maisha.
- Share na wengine wajue
Comments
Post a Comment